Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho

Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho

Kutoka kwa Abdillah bin Hakim- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho".

[Ni nzuri] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Atakayegeuka kwa moyo wake au vitendo vyake au kwa vyote viwili katika kitu ambacho anataraji manufaa au kuzuia madhara, Mwenyezi Mungu humuwakilisha katika kitu hicho ambacho amekielekea, atakayemuelekea Mwenyezi Mungu humtosheleza na humfanyia wepesi kila zito, na mwenye kumuelekea asiyekuwa yeye Mwenyezi Mungu humfungamanisha katika kitu hicho na humfedhehesha.

فوائد الحديث

Katazo la kuegemea kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ulazima wa kuegemea kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yote.

Kubainishwa madhara ya ushirikina na ubaya wa mwisho wake.

Malipo huendana na matendo.

Nikuwa malipo ya kitendo hurudi kwa mfanyaji yakiwa ya kheri au ya shari.

Kushindwa kwa mwenye kujiondoa kwa Mwenyezi Mungu na akatafuta manufaa kwa asiyekuwa yeye.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake., Matendo ya moyoni.