Nenda na viatu vyangu hivi viwili, yeyote utakayekutana naye mbele ya ukuta huu na hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi mpe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi

Nenda na viatu vyangu hivi viwili, yeyote utakayekutana naye mbele ya ukuta huu na hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi mpe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Tulikuwa tumekaa pembezoni mwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa pamoja nasi Abubakari na Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao katika kundi, akasimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake mbele yetu, akaondoka na akachelewa, tukahofia asije kudhuriwa mbele yetu, tukapatwa na hofu tukasimama, mimi nilikuwa wa kwanza kufadhaika, nikatoka nikimtafuta Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake mpaka nikafika katika ukuta wa Answari (watu wa Madina) katika ukoo wa bani Najjar, nikauzunguka ili nipate mahala mlango ulipo, sikuupata! Ghafla nikaona kimviringo kidogo kinachoingia ndani ya ukuta kutokea nje kilipo kisima, nikakifukua, nikaingia kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Akasema kwa mshangao "Nani we, Abuu Huraira?!" Nikasema: Ndiyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Nini kimekuleta?" Nikasema: Ulikuwa umekaa pamoja nasi ukasimama ukaondoka na ukachelewa kurudi, tukahofia usije kudhurika mbele yetu, tukapatwa na mfadhaiko, mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kufadhaika, nikaja katika ukuta huu, nikafukua kama anavyofukua Mbweha, na hawa watu wako nyuma yangu. Akasema: "Ewe Abuu Huraira" Na akanipa viatu vyake, Akasema: "Nenda na viatu vyangu hivi viwili, yeyote utakayekutana naye mbele ya ukuta huu na hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi mpe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi", akawa mtu wa kwanza kukutana naye ni Omari. Akasema: "Ni vya nini viatu hivi viwili ewe Abuu Huraira?" Nikasema viatu hivi ni vya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, kaniagiza navyo kuwa yeyote nitakayekutana naye na hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi nimpe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi, Omari akanipiga kibao kwa mkono wake kifuani kwangu kati ya maziwa mawili nikaangukia kisogo changu, akasema: Rudi ewe Abuu Huraira!, nikarudi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikataka kuangua kilio, akanifuatilia Omari naye akiwa nyuma yangu, nilipofika, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake "Umekuwaje ewe Abuu Huraira?" Nikasema: Nimekutana na Omari nikamueleza ulichoniagiza, akanipiga kibao kifuani kati ya maziwa yangu mawili, nikaangukia kisogo, akasema: "Rudi!" Basi akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Omari, ni nini kimekupelekea kufanya ulichokifanya?" Omari akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nakuthamini na niko radhi fidia yako kumtoa baba yangu na mama yangu, hivi ni kweli umemtuma Abuu Huraira akiwa na viatu vyako, kuwa atakayekutana naye hali yakuwa anashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo ukiwa na yakini kabisa na hilo, basi ampe habari njema kuwa yeye ni katika watu wa peponi? Akasema: "Ndiyo nimemtuma", Omari akasema: Ni bora usifanye hivyo, hakika mimi nahofia watu watabweteka na hilo, acha watende, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Basi Abuu Huraira waache".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kakaa katika kundi la Maswahaba zake, akiwa miongoni mwao Abubakari na Omari, akasimama rehema na amani ziwe juu yake akaondoka, kisha akachelewa, wakahofia asijekupatwa na kero kutoka kwa adui; ima kwa kutekwa au kinginecho. Wakasimama Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao wakiwa na mfadhaiko, akawa wa mwanzo kufadhaika ni Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake, akaondoka mpaka akafika katika Bustani ya Bani Najjari, akaanza kuizunguka huenda anaweza kupata mlango ulio wazi akawa hakuupata, lakini alipata upenyo mdogo katika ukuta yanapoingilia maji, akaukunja mwili wake mpaka akaingia akamkuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kumwambia? Akasema: Ndiyo. Akasema: Umepatwa na nini?. Abuu Huraira akasema: Ulikuwa pamoja nasi, ukasimama ukaondoka na ukachelewa, tukahofia usijekudhurika mbele yetu, nikawa mimi ndio wa mwanzo kufadhaika, nikaja katika ukuta huu, nikapenya kama anavyopenya mbweha, na hawa watu wakiwa nyuma yangu. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akampa viatu vyake kama nembo na alama kuwa yeye ni mkweli, na akasema kumwambia: Nenda na viatu vyangu hivi, utakayekutana naye nyuma ya ukuta huu, akiwa anashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na wala hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, moyo wake ukiwa na yakini nalo; atakayekuwa na sifa hii basi huyo ni katika watu wa peponi. Akawa wa kwanza kukutana naye ni Omari, akasema kumwambia: Ni vya nini viatu hivi ewe Abuu Huraira? Akasema: Hivi ni viatu vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amenituma kwavyo kwa yeyote nitakayekutana naye akishuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu moyo wake ukiwa na yakini na hilo, basi nimbashirie Pepo. Omari akapiga kifua cha Abuu Huraira kwa mkono wake akaanguka kwa nyuma, akasema: Rudi ewe Abuu Huraira, nikarudi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikiwa na mfadhaiko na uso wangu ukiwa umebadilika nikiwa nataka kulia, na Omari akanifuata na akawa anatembea nyuma yangu. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Umekuwaje ewe Abuu Huraira? Nikasema: Nimekutana na Omari, nikamueleza ulichonituma, akanipiga kipigo kikali, nikaanguka kwa nyuma, na akasema: Rudi. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ewe Omari, nini kimekupelekea kufanya hivyo? Akasema Omari: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimtoe fidia kwa ajili yako baba yangu na mama yangu, hivi ni kweli ulimtuma Abuu Huraira akiwa na viatu vyako, kwamba atakayekutana na Mwenyezi Mungu huku akishuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na moyo wake ukiwa na yakini na hilo ampe habari nje ya pepo?. Akasema: Ndiyo. Akasema: Usifanye hivyo, kwani mimi ninahofia watu watabweteka kwa kauli hiyo pekee pasina kufanya matendo, acha wafanye. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Basi waache.

فوائد الحديث

Pupa kubwa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na pupa yao juu ya usalama wake dhidi ya kila kero.

Sheria ya kutoa habari njema za kheri na zenye kufurahisha.

Imani ni kauli na matendo na itikadi.

Amesema Kadhi Iyadhi na wengineo: Na si kwamba kitendo cha Omari radhi za Allah ziwe juu yake kumwendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kupinga na kukataa amri yake; kwani hakuna katika lile aliloagizwa Abuu Huraira zaidi ya kufurahisha Umma na kuwapa habari njema, Omari radhi za Allah ziwe juu yake akaona kulificha hilo ndio kuna masilahi kwao na ndio bora zaidi ili wasibweteke, na kwamba hilo linawapa hamasa zaidi ya kufanya kheri kuliko bishara hii ya haraka, alipolifikisha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaliona kuwa ni sahihi.

Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii nikuwa kiongozi na mtu mkubwa yeyote watakapoona jambo na wafuasi wake wakaona kinyume na hivyo; ni wajibu kwa kiongozi alifikishe kwa wafuasi ili walitazame, ikiwa itabainika kuwa alichokisema kiongozi ni sahihi basi watakichukua na kama si sahihi basi kiongozi anawajibu wa kuweka wazi utata uliofikishwa kwake.

Inafaa kujizuia kutosambaza baadhi ya elimu ambazo hazina haja kwa watu kwa ajili ya masilahi au kuhofia madhara.

Bishara kubwa kwa watu wa tauhidi, na kwamba atakayekufa hali yakuwa anashuhudia kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, kwa kutakasa moyo wake katika hilo basi anasatahiki pepo.

Nguvu ya Omari radhi za Allah ziwe juu yake, na hekima yake, na upana wa uelewa wake.

Amesema Nawawi: Na hapa kuna kufaa mtu kuingilia miliki ya mtu mwingine pasina idhini yake anapojua kuwa anaridhia hilo, kwa sababu ya mapenzi yaliyo kati yao, au kinginecho.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.