Ikiwa mtapenda nitakupeni, lakini mali hii tajiri hana fungu ndani yake wala mwenye nguvu mwenye uwezo wa kuchuma mali

Ikiwa mtapenda nitakupeni, lakini mali hii tajiri hana fungu ndani yake wala mwenye nguvu mwenye uwezo wa kuchuma mali

Kutoka kwa Ubaidillah bin Adiy binil-Khiyari amesema: Walinieleza watu wawili kuwa wao walimjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Hija ya kuaga wakati akigawa sadaka, wakamuomba katika sadaka hizo, akatunyanyulia macho kisha akayashusha, akatuona ni watu shupavu wenye nguvu, akasema: "Ikiwa mtapenda nitakupeni, lakini mali hii tajiri hana fungu ndani yake wala mwenye nguvu mwenye uwezo wa kuchuma mali".

[Sahihi] [رواه أبو داود والنسائي]

الشرح

Walikuja watu wawili kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Hija ya kuaga, wakati akigawa sadaka, na wakamuomba awapatie katika sadaka hizo, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawa anawatazama mara kwa mara, ili ajue hali zao, na je, ni halali kwao kupewa sadaka au la? Akawaona ni wanaume wawili wenye nguvu, akasema: Ikiwa mtapenda nitawapa katika sadaka hizi, lakini hana fungu ndani yake mwenye mali inayomtosheleza, wala kwa mwenye uwezo wa kutafuta na kuchuma mali, hata asipokuwa na mali inayomfanya ahesabike miongoni mwa wenye uwezo.

فوائد الحديث

Ni haramu kuomba kwa mtu mwenye uwezo au mwenye nguvu ya kutafuta.

Asili kwa mtu asiyejulikana kuwa ana mali au hana, ni kustahiki kupewa sadaka.

Nguvu peke yake hazipelekei mtu kutostahiki sadaka, bali ni lazima ziambatane na uwezo wa kutafuta mali.

Mwenye uwezo wa kuchuma kiasi kinachomtosheleza haifai kwake kuchukua sadaka ya wajibu; kwa sababu amejitosheleza kwa utafutaji, ni kama kujitosheleza kwa mwenye uwezo kwa mali.

Malezi matukufu ya Mtume kwa utu wa Muislamu juu ya utukufu wa nafsi, na katika utoaji, si kupokea na kuomba na uvivu.

التصنيفات

Matumizi ya Zakkah.