Peaneni zawadi, mtapendana

Peaneni zawadi, mtapendana

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- anasema: "Peaneni zawadi, mtapendana."

[Ni nzuri (Hasan)] [Imepokelewa na Bukhari katika Al-Adab Al-Mufrad na Abuu Ya'laa na Al-Bayhaqiy]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemhimiza Muislamu kuwa abadilishane zawadi na ndugu yake Muislamu, na kuwa zawadi ni miongoni mwa sababu za mapenzi na kuziunganisha nyoyo.

فوائد الحديث

Ni sunna kutoa zawadi; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrisha kufanya hivyo.

Zawadi ni sababu ya kuleta mapenzi.

Inampasa mwanadamu afanye kila ambacho ndani yake kinaleta mapenzi kati yake na watu wengine, sawa sawa iwe ni katika zawadi au kuwa mpole, au katika maneno mazuri au katika ukunjufu wa uso kwa kadiri awezavyo.

التصنيفات

Kutoa Bure na Utoaji wabadala.