إعدادات العرض
Hawatofanikiwa watu waliomkabidhi utawala wao mwanamke
Hawatofanikiwa watu waliomkabidhi utawala wao mwanamke
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Bakra -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hawatofanikiwa watu waliomkabidhi utawala wao mwanamke".
الترجمة
العربية Bosanski English فارسی Français Русский हिन्दी 中文 Bahasa Indonesia اردو Kurdî Português دری Македонски Tiếng Việt Magyar ქართული বাংলা ไทย অসমীয়া Hausa Nederlands ਪੰਜਾਬੀالشرح
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hawatofanikiwa watu kwa kupata wanayoyataka pindi watakapomtawalisha na kummilikisha mwanamke swala la hukumu au usimamizi wa dola au wizara.فوائد الحديث
Wanawake hawasimamii uongozi wala hukumu kwa watu, na mfano wa hayo katika usimamizi wa majukumu makuu, ama mambo maalumu kama usimamizi wa mali za wakfu au mayatima au ukuu wa shule na mfano wa hayo hakuna tatizo.
Kumebainishwa udhaifu mkubwa wa mwanamke, na kwamba hashirikiani na wanaume katika usimamizi mkuu, na kwamba kusimamia kwake mfano wa majukumu hayo ni sababu ya kukosa mafanikio.
Mwenyezi Mungu alimuumba mwanamke, na akamuwekea tabia zinazotofautiana na tabia za mwanaume, kuna mambo hayafai kusimamiwa na mwanamke; kulingana na tabia yake ya kipekee, vile vile kuna mambo hayafai kusimamiwa na mwanaume; kulingana na tabia yake ya kipekee.
Kufanikiwa kulikokanushwa: Ni kufanikiwa kuliko tajwa katika ulimi wa sheria, nako ni kupatikana kwa kheri za dunia na akhera, na haimaanishi ustawi wa ufalme kuwa watu wanampendeza Mwenyezi Mungu, yeyote asiyemtii Mwenyezi Mungu si miongoni mwa waliofanikiwa, hata kama yuko katika hali nzuri zaidi katika kile kinachoonekana miongoni mwa mambo yake ya kidunia.
Hakuna maana yoyote ya kumshusha hadhi mwanamke katika hadithi hii, lakini ni maelekezo ya uwezo wake sahihi unaomfaa kwake.
التصنيفات
Masharti ya kiongozi mkuu.