Sisi ni Umma wa mwisho, na ndio wa kwanza kuhesabiwa

Sisi ni Umma wa mwisho, na ndio wa kwanza kuhesabiwa

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Sisi ni Umma wa mwisho, na ndio wa kwanza kuhesabiwa, patasemwa: Uko wapi Umma usiosoma na Nabii wao? Sisi ni wa mwisho wa mwanzo".

[Sahihi] [Imepokelewa na Ibnu Maajah]

الشرح

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Umma wake ndio Umma wa mwisho kuwepo na zama pia, na ndio Umma wa kwanza katika Umma zote utakaohesabiwa siku ya Kiyama, patasemwa siku ya Kiyama: Uko wapi Umma usiosoma na Nabii wao? Umenasibishwa katika kutojua kusoma kwake rehema na amani ziwe juu yake kwa kutojua kusoma wala kuandika. Wataanza kuitwa mwanzo kwa ajili ya hesabu, sisi ni wa mwisho katika zama za kuwepo, na wa kwanza katika kuhesabiwa siku ya Kiyama na katika kuingia Peponi.

فوائد الحديث

Ubora wa Umma huu kuliko Umma zilizotangulia.

التصنيفات

Maisha ya Akhera.