Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kikimuosha kibaba cha maji kutokana na janaba, na ukimtia udhu ujazo wa kiganja

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kikimuosha kibaba cha maji kutokana na janaba, na ukimtia udhu ujazo wa kiganja

Kutoka kwa Safina radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kikimuosha kibaba cha maji kutokana na janaba, na ukimtia udhu ujazo wa kiganja.

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akioga kutokana na janaba kwa kiasi cha kibaba, na akitawadha kwa ujazo wa kiganja, na kibaba: Ni ujazo wa viganja vinne, na kiganja: Ni kiasi cha ujazo wa viganja viwili vya mtu wa maumbile ya kati na kati.

فوائد الحديث

Sheria ya kubajeti maji ya udhu na ya kuoga, na kutofanya ubadhirifu hata kama maji ni mengi.

Kupendeza kutumia kidogo katika maji ya udhu na ya kuoga kulingana na haja, na kwamba huu ndio muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

lengo ni kueneza maji katika udhu na kuoga ikiwa ni pamoja na kuzingatia sunna na adabu, pasina kufanya ubadhirifu wala kupunja sana, na azingatie muda na wingi wa maji na uchache wake na mengineyo.

Huitwa janaba kwa kila aliyeshusha manii au aliyefanya tendo la ndoa, na limeitwa hivyo kwa sababu mtu hujitenga na swala na ibada mbali mbali mpaka asafishike.

Kibaba: Ni kipimo maarufu, na hukusudiwa kibaba cha Mtume, na kinafikia ujazo wake (480 g) za ujazo wa ngano safi, na kwa lita ni Lita (3).

Mudd (kiganja): Ni moja kati ya vipimo vya kisheria, nacho ni ujazo wa viganja viwili vya mtu wa kati na kati atakapovijaza na kunyoosha mkono wake, na kiganga kimoja ni robo kibaba, kwa itifaki ya wanachuoni, na kiasi chake ni (ml 750).

التصنيفات

Sunna na Adabu za Kutawadha, Sunna na Adabu za Kutawadha