إعدادات العرض
Itakapokimiwa swala basi hakuna swala nyingine isipokuwa swala ya faradhi
Itakapokimiwa swala basi hakuna swala nyingine isipokuwa swala ya faradhi
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Itakapokimiwa swala basi hakuna swala nyingine isipokuwa swala ya faradhi".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية Português دری Македонски Magyar Tiếng Việt ქართული বাংলা Kurdî ไทย অসমীয়া Nederlands ਪੰਜਾਬੀ Bahasa Indonesia Hausa ភាសាខ្មែរالشرح
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemkataza atakayekuwa msikitini aanze kuswali sunna baada ya kukimiwa swala ya faradhi.فوائد الحديث
Katazo la kuswali sala ya sunna itakapokimiwa swala ya faradhi msikitini.
Katazo la kuanza sunna baada ya kukimiwa swala, sawa sawa iwe ni sunna yenye utaratibu maalumu kama sunna ya Alfajiri na Adhuhuri au nyingineyo.
Pindi itakapokimiwa swala akiwa ndani ya sala ya sunna; ikiwa amebakiza kiasi kidogo chini ya rakaa moja basi ataikamilisha kwa haraka, na isipowezekana basi ataikatisha ili aipate takbira ya kuanza swala.
