Hakuwahi kuwapiga vita Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu hata siku moja isipokuwa kwanza alianza kuwaita katika Uislamu

Hakuwahi kuwapiga vita Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu hata siku moja isipokuwa kwanza alianza kuwaita katika Uislamu

Kutoka kwa bin Abbas- radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Hakuwahi kuwapiga vita Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu hata siku moja isipokuwa kwanza alianza kuwaita katika Uislamu.

[Sahihi] [رواه أحمد والبيهقي]

الشرح

Ameeleza bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yao kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwahi kuanza kuwapiga vita watu mpaka kwanza awaite katika Uislamu, wasipokubali wito wake anawapiga vita.

فوائد الحديث

Sharti la kufikisha ujumbe wa Uislamu kwanza kabla ya vita, ikiwa Uislamu haujawafikia.

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwaita katika Uislamu, wakikataa basi anawapa hiari ya kulipa kodi, wakikataa anawapiga vita, kama ilivyokuja katika hadithi zingine.

Lengo la Jihadi ni watu kuingia katika Uislamu, na si tamaa ya kuwaua na kuchukua mali zao na miji yao.

التصنيفات

Hukumu na Maswala ya Jihadi.