Basi Mwenyezi Mungu ana huruma zaidi kwa waja wake kuliko mwanamke huyu kwa mtoto wake

Basi Mwenyezi Mungu ana huruma zaidi kwa waja wake kuliko mwanamke huyu kwa mtoto wake

Imepokewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Walikuja mateka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara kukawa na mwanamke miongoni mwa mateka akikamua maziwa yake na kunyonyesha, akipata mtoto katika mateka anamchukua, anamkumbatia na kumuweka tumboni kwake na kumnyonyesha, basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kutuambia: "Hivi mnadhani mwanamke huyu anaweza kumtupa mwanaye motoni?" Tukasema: Hapana, hawezi kumtupa, akasema: "Basi Mwenyezi Mungu ana huruma zaidi kwa waja wake kuliko mwanamke huyu kwa mtoto wake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Waliletwa mateka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka katika kabila la Hawazini, mara kukawa na mwanamke miongoni mwao akimtafuta mwanaye, kila akipata mtoto anamnyonyesha kwa sababu ya kudhurika kwake kwa wingi wa maziwa katika matiti yake, mara, akampata mwanaye katika mateka akamchukua, akamkumbatia tumboni kwake na akamnyonyesha, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwaambia Maswahaba zake: Hivi mnadhani mwanamke huyu anaweza kumtupa mwanaye motoni? Tukasema: Kamwe, hawezi kumtuka kwa hiyari yake milele. Akasema: Basi Mwenyezi Mungu ana huruma zaidi kwa waja wake Waislamu kuliko mwanamke huyu kwa mtoto wake.

فوائد الحديث

Huruma pana ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwamba yeye anawatakia mema na Pepo, na kusalimika na Moto.

Kunufaika na matukio na kuyafungamanisha na kutoa maelekezo na mafunzo.

Inampasa muumini awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu, na wala asikate tamaa, ikiwa ni pamoja na kumcha Mwenyezi Mungu na kuwa na msimamo katika dini yake, kwani Yeye Mtukufu Ndiye Mwenye huruma pana zaidi.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.