Yakwamba Mtume rehema na Amani zimfikie aliulizwa kuhusu Nushra (kutibu uchawi kwa uchawi)? Akasema: Hiyo ni katika kazi za shetani.

Yakwamba Mtume rehema na Amani zimfikie aliulizwa kuhusu Nushra (kutibu uchawi kwa uchawi)? Akasema: Hiyo ni katika kazi za shetani.

Kutoka kwa Jaabir radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-Yakwamba Mtume rehema na Amani zimfikie aliulizwa kuhusu Nushra (kutibu uchawi kwa uchawi)? Akasema: Hiyo ni katika kazi za shetani.

[Sahihi] [Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Nikuwa Mtume rehema na Amani ziwe juu yake - Aliulizwa kuhusu kumtibu aliyerogwa kwa njia ambayo walikuwa wakiijua tangu zama za ujinga, mfano: kuondoa uchawi kwa uchawi ni ipi hukumu ya hilo, akajibu rehema na Amani zimfikie kuwa hiyo ni katika kazi za shetani, au hufanyika kupitia yeye; kwasababu inakuwa kwa aina ya uchawi na kwa kuwatumia mashetani, hiyo ni ushirikina na ni haramu. na ama kutibu uchawi kunakofaa: ni kuufungua uchawi kwa kisomo cha ruqya au kuutafuta, na kuufungua kwa mkono pamoja na kusoma Qur'ani au kwa dawa za halali.

فوائد الحديث

Sheria ya kuwauliza wanachuoni katika yale yanayotatiza hukumu yake; kwa tahadhari ya kutoangukia katika haramu.

Katazo la kutibu uchawi kwa namna wanayoifahamu watu wa zama za ujinga; kwasababu ni uchawi na uchawi ni ukafiri.

Nikuwa kazi za shetani zote zimeharamishwa.

التصنيفات

(Mambo ya kale kabla ya uislamu), Ushirikina.