Madhambi makubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kujiaminisha na adhabu za Mwenyezi Mungu, na kukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, Na kufa moyo katika huruma za Mwenyezi Mungu

Madhambi makubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kujiaminisha na adhabu za Mwenyezi Mungu, na kukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, Na kufa moyo katika huruma za Mwenyezi Mungu

Kutoka kwa Abdillahi bin Masoud Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake yakwamba yeye amesema: "Madhambi makubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kujiaminisha na vitimbi vya Mwenyezi Mungu, na kukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, Na kufa moyo katika huruma za Mwenyezi Mungu".

[upokezi wake ni sahihi] [Imepokelewa na Abdul Razaaq]

الشرح

Ametaja Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii madhambi ambayo yanazingatiwa kuwa ni katika madhambi makubwa, nayo: ni kuwekewa Mwenyezi Mungu Mtukufu mshirika katika uumbaji wake na kuabudiwa kwake, na ameanza na hili, kwasababu ndiyo dhambi kubwa kuliko yote, na kukata matarajio na matumaini kwa Mwenyezi Mungu; kwasababu huko ni kumdhania vibaya Mwenyezi Mungu na ni kutojua upana wa rehema zake, na kujiaminisha kwa kumvuta taratibu mja kwa kumpa neema ili mpaka aje kumchukua akiwa kaghafilika, na si makusudio ya hadithi kudhibiti idadi ya madhambi makubwa kuwa hakuna zaidi ya haya yaliyotajwa, lakini makusudio yake ni kubainisha makubwa yake.

فوائد الحديث

Kugawanyika kwa madhambi makubwa na madogo

Nikuwa ushirikina ni dhambi kubwa na ni kosa kubwa kuliko yote.

Uharamu wa kujiaminisha na vitimbi vya Mwenyezi Mungu Mtukufu- na kukata tamaa na rehema zake, nakuwa hayo ni katika madhambi makubwa.

Kufaa kumsifu Mwenyezi Mungu kwa vitimbi katika kupambana na wenye vitimbi, na hii ni sifa ya ukamilifu, na sifa mbaya ni vitimbi kwa asiyestahiki kufanyiwa vitimbi.

Nikuwa la msingi kwa mja awe kati ya hofu na kutaraji, akiwa na hofu hawezi kukata tamaa, na akitaraji hawezi kujiaminisha.

Kuthibitisha sifa ya huruma kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa namna inayoendana na Utukufu wake.

Ulazima wa kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu Mtukufu.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.