Mlisheni mwenye njaa, na mtembeleeni mgonjwa, na mwacheni huru mateka

Mlisheni mwenye njaa, na mtembeleeni mgonjwa, na mwacheni huru mateka

Imepokewa kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mlisheni mwenye njaa, na mtembeleeni mgonjwa, na mwacheni huru mateka".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika haki za Muislamu kwa ndugu yake Muislamu ni kumlisha mwenye njaa na kumtembelea mgonjwa, na kumuacha huru mateka.

فوائد الحديث

Himizo la Waislamu kusaidizana.

Himizo la kumlisha chakula mwenye njaa na uhitaji, huyu imeamrishwa kumlisha.

Sheria ya kumtembelea mgonjwa; ili kumpa faraja, na kumuombea dua na kupata malipo, na mengineyo.

Kufanya pupa kumwacha huru mateka aliyetekwa na makafiri, na hiyo ima kwa kulipa gharama inayohitajika ili kumuondoa mikononi mwao, au kwa kubadilisha nao na mateka wa kikafiri, yaani: Kwa njia ya kubadilishana.

التصنيفات

Tabia njema.