إعدادات العرض
Tabia njema.
Tabia njema.
1- Atakapompenda mtu ndugu yake basi na amueleze kuwa anampenda
2- Allah amhurumie mtu ambaye ni mpole anapouza, na anaponunua, na anapo dai deni
4- Mche Mwenyezi Mungu popote ulipo, na ovu lifuatishe jema litalifuta, na ishi na watu kwa tabia njema
5- Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu
6- Usikasirike
8- Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote
9- Kamwe!, Usidharau chochote katika wema, hata kama ni kukutana na ndugu ukiwa na uso mkunjufu
11- Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake
12- Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze
13- Asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii
17- Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama
18- Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja mchamungu, mwenye kutosheka, mnyenyekevu
20- Hakika upole hauwi ndani ya kitu isipokuwa hukipendezesha, na hautolewi ndani ya kitu ila hukichafua
21- Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku
22- Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote
25- Hatomsitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya kiyama
28- Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake
31- Muumini si msemaji watu vibaya wala mtoaji wa laana wala muovu wala mwenye kauli chafu
