Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake

Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa imani kamili ya Muislamu yeyote haikamiliki mpaka ampendelee nduguye anachokipenda yeye, katika matendo mema, na aina mbalimbali za wema katika dini na dunia, na achukie kwake kinachochukiwa na nafsi yake, na ikiwa ataona kwa ndugu yake Muislamu kuna upungufu katika dini yake, basi ajitahidi kurekebisha, na akiona kuna jambo la kheri basi amtie moyo na amsaidie, na amnasihi katika dini yake au mambo ya dunia yake.

فوائد الحديث

Ulazima wa mtu kumpendelea ndugu yake kile anachokipenda kwa nafsi yake. Kwa sababu kukanushwa imani kwa mtu ambaye hampendelei ndugu yake kile anachopenda yeye mwenyewe kunaonyesha ulazima wa hilo.

Udugu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu uko juu zaidi kuliko udugu wa nasaba (ukoo), kwani haki yake ni wajibu.

Katazo la maneno na vitendo vyote vinavyopingana na upendo huu, kama vile udanganyifu, kusengenya, husuda, na uadui dhidi ya mtu, au mali yake, au heshima yake.

Kutumia baadhi ya maneno yanayotia hamasa ya kufanya matendo; kwa kauli yake "Kwa ndugu yake".

Amesema Al-Kirmani, Mwenyezi Mungu amrehemu: Pia ni sehemu ya imani kuchukia kwa ndugu yake uovu anaouchukia kwa nafsi yake, na hili (Mtume) hakulitaja, kwa sababu kukipenda kitu kunalazimu kuchukia kinyume chake, hivyo kuacha kutolisema hilo inatosha.

التصنيفات

Tabia njema.