Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake

Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake

Kutoka kwa Abuu Masoud Al-Answari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika kipandwa changu kimeangamia nakuomba msaada wa usafiri, akasema: "Sina uwezo" Mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuonyesha kwa mtu atakayeweza kumbeba, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika mimi kimeangamia kipandwa changu, nipe msaada, na unipe kipandwa kitakachonifikisha, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akampa udhuru yakuwa yeye hana kitu cha kumsaidia, mtu mmoja akasema na alikuwepo katika mazungumzo: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuelekeza kwa mtu atakaye mbeba, akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atashiriki katika kupata malipo na mtoaji, kwa sababu amemuelekeza muhitaji kwake.

فوائد الحديث

Himizo la kuelekeza katika kheri.

Himizo la kufanya kheri ni katika sababu za kuinyanyua jamii ya kiislamu na kutoshelezana.

Upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Hadithi hii ni kanuni kuu, yanaingia hapa matendo yote ya kheri.

Mtu atakaposhindwa kutimiza hitajio la muombaji, basi amuelekeze kwa mwingine.

التصنيفات

Tabia njema.