Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote

Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote

Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakuwa na maneo machafu wala mwenye kuyatafuta, na alikuwa akisema: "Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Haikuwa katika tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa na maneno machafu, au vitendo vibaya, na hakuwa anayataka hayo wala kuyatafuta kwa makusudi, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwenye tabia tukufu. Na alikuwa -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Hakika mbora wenu mbele ya Allah ni mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wote, kwa kutenda wema, na kuwa na uso mkunjufu, na kuacha maudhi na kuyavumilia, na kujichanganya pamoja na watu kwa yale mazuri.

فوائد الحديث

Ni lazima kwa muumini ajiweke mbali na maneno machafu na vitendo vibaya.

Ukamilifu wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hayatokei kwake ila matendo mema na maneno mazuri.

Tabia njema ni uwanja wa mashindano, atakayeshinda atakuwa ni muumini bora na mwenye imani iliyokamilika zaidi kuliko wote.

التصنيفات

Tabia njema.