Haya ni katika imani

Haya ni katika imani

Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- siku moja alimsikia mtu mmoja akimnasihi ndugu yake kuhusu haya (Aibu) akasema: "Haya ni katika imani".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimsikia mtu mmoja akimnasihi ndugu yake aache kuwa na aibu sana! akambainishia kuwa haya ni katika imani, nakuwa huwa haiji ila kwa kheri. Na haya ni tabia inayomsukuma mtu kufanya zuri na kuacha baya.

فوائد الحديث

Kinachokuzuia kufanya kheri hakiitwi kwa jina la haya, bali kitu hicho kinaitwa uoga na kushindwa na kufeli na hofu.

Kumuonea haya Mwenyezi Mungu Mtukufu kunakuwa kwa kufanya maamrisho, na kuacha maharamisho.

Kuwaonea haya viumbe kunakuwa kwa kuwaheshimu, na kumpa kila mtu nafasi yake, na kuyapuke yanayotia dosari siku zote.

التصنيفات

Tabia njema.