Hakika katika yale waliyoyakuta watu miongoni mwa maneno ya kiutume ya mwanzo, usipokuwa na haya basi fanya ulitakalo

Hakika katika yale waliyoyakuta watu miongoni mwa maneno ya kiutume ya mwanzo, usipokuwa na haya basi fanya ulitakalo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika katika yale waliyoyakuta watu miongoni mwa maneno ya kiutume ya mwanzo, usipokuwa na haya basi fanya ulitakalo".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika yale yaliyokuja na usia ndani yake kutoka kwa Manabii waliotangulia, na yakaenea kwa watu na watu wakarithishana kutoka kwao karne baada ya karne, mpaka yakamfikia wa mwanzo katika umma huu, ni; tazama unayotaka kuyafanya, ikiwa yatakuwa ni katika mambo ambayo si aibu basi fanya, na ikiwa ni katika mambo ya aibu basi acha; kwa sababu kinachozuia kufanya matendo mabaya ni haya, atakayekosa aibu basi hutumbukia katika kila machafu na maovu.

فوائد الحديث

Kuwa na Haya ndio asili ya tabia njema.

Haya ni sifa miongoni mwa sifa za Manabii amani iwe juu yao, nayo ni katika mambo yaliyopokelewa kutoka kwao.

Haya ni ile inayomfanya muislamu kufanya yanayompa muonekano mzuri na wa kupendeza, na kuacha yanayomchafua na kuharibu muonekano.

Amesema Imam Nawawi: Amri iliyoko ndani yake ni ya uhalali, maana yake: Ukitaka kufanya jambo, ikiwa ni jambo ambalo hutoona haya kwa Mwenyezi Mungu au kwa watu, basi lifanye, vinginevyo usifanye, na huu ndio mwenendo wa Uislamu, na muongozo wa hayo ni kuwa amri zote na wajibu na sunna, ni aibu kuziacha, na yaliyokatazwa na haramu na haya ni aibu kuyafanya, na ama ya halali kuona haya kuifanya inajuzu, na vile vile kuiacha, Hadithi hii imekusanya hukumu tano, na imesemwa kuwa: Ni amri ya kutishia, na maana yake nikuwa: Iwapo staha itaondolewa, basi fanya chochote unachotaka; kwani Mwenyezi Mungu atakulipa kwa hilo, na ikasemwa kuwa: Ni amri kwa maana ya habari, maana yake: Asiyekuwa na haya anafanya apendavyo.

التصنيفات

Tabia njema.