إعدادات العرض
Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote
Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote
Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote"
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Kurdî Português தமிழ் አማርኛ অসমীয়া ગુજરાતી Nederlands پښتو नेपाली Hausa മലയാളം Svenska ไทย Кыргызча Română Malagasy ಕನ್ನಡ Српски తెలుగు ქართული Mooreالشرح
Anatueleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kunyimwa upole akawa hakuafikishwa katika mambo ya dini na dunia, na katika mambo yake mwenyewe, na yale anayoyafanya na wengine, basi atakuwa kanyimwa kheri yote.فوائد الحديث
Fadhila za upole na himizo la kujipamba na tabia hiyo, na kemeo la ukali.
Upole hunyoosha kheri za Dunia na Akhera na hupanua mlango wa baraka, lakini ukali ni kinyume chake.
Upole ni taji ambalo hutokana na tabia njema na amani, na jeuri hutokana na hasira na ufidhuli, ndio maana aliusifia sana upole Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akapitiliza katika kusifu.
Alisema Sufian Al-Thauri Mwenyezi Mungu amrehemu, akiwaambia jamaa zake: Je, mnajua upole ni nini? Ni kuweka mambo mahali pake panapofaa, na ukali mahali pake panapofaa, na upole mahali pake panapofaa, upanga mahali pake panapofaa, na mjeledi mahali pake.
التصنيفات
Tabia njema.