Je, nisikuelezeni mbora wenu na muovu wenu?

Je, nisikuelezeni mbora wenu na muovu wenu?

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisimama kwa watu waliokaa, akasema: "Je, nisikuelezeni mbora wenu na muovu wenu?" Anasema: Wakanyamaza, akalisema hilo mara tatu, mtu mmoja akasema: Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tueleze mbora wetu na muovu wetu, akasema: "Mbora wenu ni yule inayetarajiwa heri yake, na kuaminiwa kutokuwepo kwa shari yake, na muovu wenu ni yule isiyetarajiwa heri yake, na kutoaminiwa shari yake".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Alisimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake mbele za watu waliokaa miongoni mwa Maswahaba zake akawauliza, je nisikuelezeni na nikumbusheni ni nani mbora wenu na ni nani muovu wenu? Wote hawakuzungumza na wala hawakujibu chochote, kwa kuhofia kubainishwa mbora wao na muovu wao na wakahofia fedheha wakanyamaza. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akarudia swali mara tatu, akajibu mtu mmoja miongoni mwao: Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tueleze mbora wetu na muovu wetu. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawabainishia: Kuwa mbora wenu ni yule inayesubiriwa na kutarajiwa heri yake na ihisani yake na wema wake, na kuaminiwa kutowepo shari yake kusiogopwe uadui wake na uonevu wake na dhuluma yake, na kuwa muovu wenu ni yule asiyetarajiwa wala kusubiriwa wala kutamaniwa kupatikana heri yake na ihisani yake na wema wake, na haiaminiwi shari yake, bali unahofiwa uadui wake na uonevu wake na dhuluma yake.

فوائد الحديث

Kumebainishwa mtu bora na mtu muovu.

Manufaa na madhara yenye kuvuka kwenda kwa watu wengine ni makubwa kuliko yanayoishia kwa mtu binafsi.

Himizo la kuwa na tabia njema, na kuamiliana vizuri na watu, na tahadhari ya uovu na shari na uadui.

التصنيفات

Tabia njema.