Hakika waadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika mimbari za nuru, kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake yote miwili ni kulia

Hakika waadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika mimbari za nuru, kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake yote miwili ni kulia

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika waadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika mimbari za nuru, kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake yote miwili ni kulia , wale wanaofanya uadilifu katika hukumu zao na familia zao, na vile wanavyovitawala"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wanaohukumu kwa uadilifu na haki baina ya watu walio chini ya utawala wao na hukumu zao, na familia zao, nikuwa watakaa katika makao ya juu zaidi yaliyoumbwa kwa nuru, ikiwa ni takrima kwao siku ya Kiyama. Na mimbari hizi ziko kuliani mwa Allah Mtukufu, na mikono yake miwili Mtukufu yote ni kulia.

فوائد الحديث

Fadhila za uadilifu na himizo juu yake.

Uadilifu ni neno la kiujumla linalokusanya tawala zote, na hukumu za kati ya watu hata uadilifu kati ya wake na watoto, na mengineyo.

Kumebainishwa nafasi ya waadilifu siku ya Kiyama.

Kutofautiana kwa makazi ya watu wa imani siku Kiyama kila mmoja atakuwa kulingana na matendo yake.

Mfumo wa kuhamasisha ni katika njia za kufanya da'wa zinazomvutia mwenye kulinganiwa kuja katika utiifu.

التصنيفات

Tabia njema., Tabia njema.