Hana imani asiyekuwa na uaminifu, na hana dini asiyekuwa na ahadi (za kweli)

Hana imani asiyekuwa na uaminifu, na hana dini asiyekuwa na ahadi (za kweli)

Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Hakuwahi kutuhutubia sisi Mtume rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa alisema: "Hana imani asiyekuwa na uaminifu, na hana dini asiyekuwa na ahadi (za kweli)".

[Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyingine] [Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kuwa ni mara chache sana akihutubia Mtume rehema na amani ziwe juu yake au atoe mawaidha isipokuwa alikuwa akitaja mambo mawili: La kwanza: Hana imani mtu ambaye ndani ya nafsi yake kuna hiyana na mtu katika mali yake au nafsi yake au familia yake. La pili: Hana dini kamili mwenye kufanya hiyana katika ahadi na mikataba na kuivunja.

فوائد الحديث

Himizo la kutekeleza amana na kutimiza ahadi, kwani kuivunja hupunguza imani.

Tahadhari ya kutofanya hiyana na kuvunja ahadi, na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa.

Hadithi hii inakusanya kutunza amana na ahadi zilizo kati ya Mwenyezi Mungu na mja wake, na zile zilizo kati ya viumbe wao kwa wao.

التصنيفات

Tabia njema.