إعدادات العرض
Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa
Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa
Kutoka kwa Abuu Abdillah Al-Jadali amesema: Nilimuuliza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa.
الترجمة
العربية Bosanski English فارسی Français Русский 中文 हिन्दी Bahasa Indonesia اردو Hausa Kurdî Tiếng Việt অসমীয়া Nederlandsالشرح
Aliulizwa mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Haikuwa katika tabia zake uchafu na ubaya wa kauli na vitendo, na wala hakuwa akijilazimisha machafu wala kuyakusudia, wala hakuwa mpiga kelele kwa kunyanyua sauti yake masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya; lakini alikuwa akilipa ubaya kwa wema, na akisamehe ndani ya moyo, na akifuta kosa na kulipuuza katika dhahiri.فوائد الحديث
Kumebainishwa tabia alizokuwa nazo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, tabia za juu na kuwa kwake mbali na tabia mbaya.
Himizo la kufanya tabia njema na kujiweka mbali na tabia mbaya.
Kumekemewa kujilazimisha machafu katika kauli na maneno machafu.
Kumekemewa kunyanyua sauti juu ya watu na kuwapigia makelele.
Himizo la kuukabili ubaya kwa wema, na kusamehe na kufuta kosa.