Na hakika Mwenyezi Mungu ameniteremshia wahyi kuwa, kuweni wanyenyevu, mpaka asijikweze yeyote kwa mwingine, na wala asimfanyie uadui yeyote mwenzake

Na hakika Mwenyezi Mungu ameniteremshia wahyi kuwa, kuweni wanyenyevu, mpaka asijikweze yeyote kwa mwingine, na wala asimfanyie uadui yeyote mwenzake

Kutoka kwa Iyaadh bin Himari ndugu yao na Bani Mujashii radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alisimama kwetu Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake siku moja kwa ajili ya kuhutubia, akasema: Na akaeileza hadithi na ndani yake alisema: "Na hakika Mwenyezi Mungu ameniteremshia wahyi kuwa, kuweni wanyenyevu, mpaka asijikweze yeyote kwa mwingine, na wala asimfanyie uadui yeyote mwenzake"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Maswahaba zake wakati akihutubia, na ikawa miongoni mwa yale aliyosema ni: Hakika Mwenyezi Mungu amemteremshia wahyi ya kwamba ni wajibu kwa watu wanyenyekeane wao kwa wao, na hii ni kwa kushusha mbawa (kujishusha) kwa viumbe na kuwa wapole, mpaka asijikweze kwa kudai ukubwa na kiburi na utukufu yeyote kwa ukoo wake au mali yake au kinginecho juu ya yeyote, na wala asidhulumu na asifanye uadui yeyote kwa mwenzake.

فوائد الحديث

Katika hadithi kuna himizo la kuwa wanyenyekevu na kutokuwa na kiburi na kujikweza juu ya watu.

Katazo la uadui na ufahari.

Kujinyenyekeza kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kuna maana mbili: Maana ya kwanza: Ni mtu unyenyekee kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu, usijikweze katika dini, na wala usiwe na kiburi, na kutekeleza hukumu zake. Na ya pili: Ni unyenyekee kwa waja wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, si kwa sababu ya kuwaogopa, na wala si kwa kutaraji walivyonavyo, lakini ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.

التصنيفات

Tabia njema., Matendo ya moyoni.