Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli chafu

Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli chafu

Kutoka kwa Abuu Dardai Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli chafu".

[Ni sahihi kwa riwaya zake mbili] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama katika kauli na matendo ni tabia njema, na hii ni kwakuwa na uso mkunjufu, na kujizuia na maudhi, na kutenda wema. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anamchukia mtu muovu katika kauli zake na vitendo, mwenye mdomo mchafu katika yale yanayotamkwa na ulimi wake.

فوائد الحديث

Ubora wa tabia njema; kwa sababu humletea mwenye nayo mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na mapenzi ya waja wake, nalo ndilo jambo kubwa katika yale yatakayopimwa siku ya Kiyama.

التصنيفات

Tabia njema., Adabu ya mazungumzo na kunyamaza.