Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema

Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: "Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema", na akaulizwa kuhusu mambo yatakayowaingiza watu motoni kwa wingi akasema: "Mdomo na utupu".

[Ni nzuri na nisahihi]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa sababu kubwa zinazowapeleka watu peponi ni mbili: Uchamungu na tabia njema. Uchamungu: Ni mtu kuweka kinga kati yako na adhabu ya Mwenyezi Mungu, nako ni kwa kufanya maamrisho yake na kuyaepuka makatazo yake. Na tabia njema: Inakuwa kwa kukunjua uso na kutenda wema na nakujizuia na kero. Na sababu kubwa zinazowaingiza watu motoni ni mbili nazo ni: Ni ulimi na utupu. ulimi miongoni mwa maasi yake: Ni uongo, kusengenya, kuchonganisha, na mengineyo. Na utupu katika maasi yake: Ni zinaa na kulawiti na mengineyo.

فوائد الحديث

Kuingia peponi kuna sababu zake ambazo zinaambatana na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwake: Ni kumcha yeye, na sababu zinazohusiana na watu, kama: Tabia njema.

Hatari ya ulimi kwa mtu, nakuwa ni katika sababu za kuingia motoni.

Hatari ya matamanio na machafu kwa mwanadamu, nakuwa hayo ni katika sababu kubwa za kuingia motoni.

التصنيفات

Tabia njema., Sifa za pepo na moto.