إعدادات العرض
Hakika katika watu wanaopendeka zaidi kati yenu kwangu mimi, na atakayekaa karibu zaidi kati yenu na mimi siku ya Kiyama ni yule atakayekuwa na tabia njema zaidi kati yenu
Hakika katika watu wanaopendeka zaidi kati yenu kwangu mimi, na atakayekaa karibu zaidi kati yenu na mimi siku ya Kiyama ni yule atakayekuwa na tabia njema zaidi kati yenu
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika katika watu wanaopendeka zaidi kati yenu kwangu mimi, na atakayekaa karibu zaidi kati yenu na mimi siku ya Kiyama ni yule atakayekuwa na tabia njema zaidi kati yenu, na hakika ninaowachukia zaidi kati yenu na watakaokaa mbali zaidi na mimi siku ya Kiyama ni watu wenye maneno mengi, na waropokaji, na wenye kujifakharisha, wakasema: Tushajua maana ya watu wenye maneno mengi na waropokaji, nini maana ya wenye kujifakharisha? Akasema: "Ni wale wenye kiburi".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල ئۇيغۇرچە Kurdî தமிழ் অসমীয়া Nederlandsالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa miongoni mwa wale wanaowapendeka zaidi kati yenu kwake katika dunia, na wa karibu zaidi katika kikao miongoni mwenu siku ya Kiyama, ni yule mwenye tabia nzuri zaidi yenu, na kuwa anayechukiwa zaidi miongoni mwenu kwake katika dunia, na atakayekuwa mbali zaidi miongoni mwenu katika kikao siku Kiyama ni mwenye tabia mbaya zaidi miongoni mwenu; "Wenye maneno mengi" wenye kukithirisha maneno kwa kukijilazimisha na kwa kutoka katika haki, "na wenye kuzama zaidi" wenye kuzungumza maneno kwa upana kwa kujitia ufasaha na kwa kuyatukuza maneno yao pasina kuchukua tahadhari wala kuchunga, "na wenye kujitia kujua" wakasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwisha wajua wenye maneno mengi na wenye kuzama zaidi, ni wapi wenye kujifanya kujua? Akasema: Ni wenye kiburi wenye kuwakejeli watu, wale wenye kuzungumza kwa upana katika maneno yao, na hufungua vinywa vyao kwa wingi wa maneno.فوائد الحديث
Tabia njema ni miongoni mwa sababu za kupendwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kuwa karibu naye siku ya Kiyama, na tabia mbaya ni kinyume na hivyo.
Tabia njema ni miongoni mwa sababu za watu kupendana wao kwa wao, na tabia mbaya kinyume na hivyo.
Himizo la kuwa na tabia njema na unyenyekevu na kutokuwa na ususuwavu na kujikalifisha.
Tahadhari ya kuzungumza kwa wingi na kiburi na kujikweza na kujikalifisha.
التصنيفات
Tabia njema.