إعدادات العرض
Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake
Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake".
[Ni nzuri]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt ئۇيغۇرچە Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు မြန်မာ ไทย Deutsch 日本語 پښتو অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands සිංහල தமிழ் دری Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy Română Kinyarwanda नेपाली Српски Wolof Soomaali Moore Українська Български Azərbaycan ქართული тоҷикӣ bm Oromoo Македонскиالشرح
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba mtu aliyekamilika zaidi kiimani ni yule itakayekuwa nzuri tabia yake, na hii kwa kuwa na uso mkunjufu, na kutenda mema, na maneno mazuri, na kuacha maudhi. Na muumini bora kuliko wote ni yule mbora kwa wake zake, kama mke wake na mabinti zake na dada zake na ndugu zake wengine wa kike; kwa sababu wao ndio watu wenye haki zaidi kutendewa tabia nzuri.فوائد الحديث
Ubora wa tabia njema nakuwa tabia njema ni katika imani.
Matendo ni katika imani, na imani huzidi na kupungua.
Heshima ya Uislamu kwa mwanamke na himizo la kumtendea wema.