إعدادات العرض
Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile litakalokukereketa katika kifua chako, na ukachukia watu wasilione
Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile litakalokukereketa katika kifua chako, na ukachukia watu wasilione
Kutoka kwa Nawwasi bin Samaan Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu wema na dhambi, akasema: "Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile litakalokukereketa katika kifua chako, na ukachukia watu wasilione".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Français Hausa Kurdî Português සිංහල Русский Nederlands Tiếng Việt অসমীয়া ગુજરાતી አማርኛ پښتو ไทย മലയാളം नेपालीالشرح
Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu wema na dhambi, akasema: Kubwa kabisa katika wema ni tabia njema pamoja na Allah, kwa kumcha, na pamoja na watu, kwa kuvumilia kero, na kupunguza hasira, na kukunjua uso, na kuwa na maneno mazuri, na kuunga udugu na kutii na kuwa mpole na kutenda wema, na kuishi vizuri na familia, na kusuhubiana na watu vizuri. Na ama dhambi ni kila kitakachokereketa ndani ya nafsi katika mambo yenye kutatiza, na kifua kikakosa utulivu na kutokunjuka, na moyo ukapata shaka, na ukaogoga kwa sababu ni dhambi, na ukawa hukutaka kulidhihirisha kwa mtu au hadharani mbele za watu kwakuwa ni baya, na hii ni kwa sababu nafsi hupenda watu waone yale mazuri yake, ikiwa itachukia watu kuyaona baadhi matendo yake basi hayo ndiyo madhambi wala hayana kheri ndani yake.فوائد الحديث
Himizo la kuwa na tabia njema; kwa sababu tabia njema ni katika mambo makubwa ya wema.
Haki na batili haviwezi kumchanganya muumini, bali anaijua haki kwa nuru aliyonayo ndani ya moyo wake, na anaichukia batili na kuikataa.
Miongoni mwa alama za dhambi ni moyo kukosa utulivu na kuwa na shaka, na kuchukia watu wasilione.
Amesema As-Sanadi: Hii ni katika mambo yenye kutatiza ambayo watu hawajui kutofautisha moja kati ya pande mbili; na kama si hivyo basi kilichoamrishwa na sheria pasina kuonekana dalili ndani yake ni kinyume na hilo katika wema, na yaliyokatazwa hivyo hivyo miongoni mwa madhambi, na hayo hakuna haja ya kuuliza ama kuutazama moyo na kuona utulivu wake.
Wanaosemeshwa katika hadithi hii ni wale wenye maumbile salama (ambao mioyo yao na akili zao hazijavurugwa na fikra potofu), na si wenye mioyo iliyofunikwa isiyojua jema wala kulikataa ovu isipokuwa yale iliyonyweshwa katika matamanio yake.
Amesema Attwayibi: Inasemekana: Imefasiriwa maana ya wema katika hadithi kwa maana nyingi, akaifasiri katika baadhi ya sehemu kuwa ni yale ambayo nafsi imetulizana kwayo na moyo ukatuliza pia, na akaifasiri katika sehemu nyingine kuwa ni imani, na katika sehemu nyingine, kwa yale yanayokuweka karibu na Mwenyezi Mungu, na hapa ameifasiri kwa kuwa na tabia njema, na akafasiri tabia njema kuwa: Ni kuvumilia maudhi na kupunguza hasira, na kukunjua uso, na kuwa na maneno mazuri, na yote hayo yanakaribiana katika maana.