Hatomsitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya kiyama

Hatomsitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya kiyama

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hatomsitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya kiyama"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu hatomsitiri ndugu yake katika jambo miongoni mwa mambo, isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atamsitiri siku ya Kiyama; kwani malipo huendana na matendo, na stara ya Mwenyezi Mungu kwake inakuwa kwa kuzisitiri aibu zake na maasi yake kwa kutoyatangaza mbele ya umati wa siku ya Kiyama, na huenda inawezakuwa kwa kutoyahesabu na kutomkumbusha.

فوائد الحديث

Sheria ya kumsitiri muislamu anapofanya maasi, pamoja na kumkemea, na kumnasihi, na kumhofisha kwa Mwenyezi Mungu, ama akiwa ni katika watu wa shari na uovu wenye kutangaza wazi maasi na uovu, hawa haitakiwi kusitiriwa; kwa sababu kuwasitiri kunawapa ujasiri wa kufanya maasi, bali wanatakiwa kushitakiwa katika mamlaka husika, hata kama watatajwa kwa majina; kwa sababu mtu anakuwa katangaza wazi yeye mwenyewe maovu yake na maasi yake.

Himizo la kusitiri aibu za watu wengine.

Miongoni mwa faida za kusitiri: Ni kumpa fursa mkosefu ya kuirejea nafsi yake na atubie kwa Mwenyezi Mungu; kwa sababu kutangaza aibu na fedhehe ni katika kueneza maovu, na kunaharibu hali ya hewa ya jamii, na kunawahadaa watu kuendelea kuyatenda.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake., Tabia njema.