Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama

Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama

Imepokewa kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama".

[Sahihi]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeitetea heshima ya ndugu yake muislamu akiwa hayupo (katika mazungumzo) kwa kukataza watu kumsema vibaya na kumkosea adabu, basi naye Mwenyezi Mungu ataizuia adhabu kwake siku ya Kiyama.

فوائد الحديث

Katazo la kuzungumza kuhusu heshima za waislamu.

Malipo huendana na matendo, atakayeirudisha heshima ya ndugu yake Mwenyezi Mungu naye atauzuia moto kwake.

Uislamu ni dini ya udugu na kuteteana kati ya waislamu.

التصنيفات

Mambo mazuri na Adabu- Heshima., Tabia njema.