إعدادات العرض
Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu
Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu
Imepokelewa kutoka kwa Abdillah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt Hausa Kurdî Português සිංහල Svenska ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ئۇيغۇرچە پښتو অসমীয়া دری Malagasy or Čeština नेपाली Oromoo Română Nederlands Soomaali తెలుగు ไทย Српски മലയാളം Кыргызча Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Wolof Magyar ქართული Moore Українськаالشرح
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa muislamu mwenye Uislamu kamili ni yule waliosalimika waislamu kutokana na ulimi wake, hawatukani, na wala hawalaani, wala hawasengenyi, na wala hawazunguki kwa aina yoyote miongoni mwa aina za maudhi kwa ulimi wake, na wamesalimika kutokana na mkono wake, hawatendei ubaya, na wala hachukui mali zao pasina haki, na mfano wa hayo, na mwenye kuhama, ni yule mwenye kuacha yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.فوائد الحديث
Ukamilifu wa Uislamu hauwi isipokuwa kwa kutofanyia maudhi watu wengine, kwa vitendo au kwa hila yoyote.
Ametaja ulimi na mkono pekee pasina viungo vingine; kwa sababu ya wingi wa makosa yake na madhara yake, kwani shari nyingi hutokea kupitia viwili hivi.
Himizo la kuacha maasi na kushikamana na yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Muislamu bora kuliko wote ni yule mwenye kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waislamu.
Uadui unaweza kuwa kwa kauli au kitendo.
Kuhama kuliko kamilika ni kuyahama aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.