Usikasirike

Usikasirike

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba mtu mmoja alisema kumwambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Niusie, akasema: " Usikasirike" Akarudia mara kadhaa, akasema: "Usikasirike".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Mmoja kati ya Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amjulishe katika jambo litakalomnufaisha, akamuamrisha asikasirike, na maana ya hapa nikuwa aziepuke sababu zinazoweza kumpelekea katika kukasirika, na aidhibiti nafsi yake na hasira zinapompata, asiendelee na hasira zake mpaka kufikia kuuwa au kupiga au kutoa matusi na mfano wa hayo. Na yule bwana akarejea tena kuomba usia mara kadhaa, hakumzidishia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika usia zaidi ya "Usikasirike"

فوائد الحديث

Tahadhari dhidi ya hasira na sababu zake, kwani ndio chanzo kikuu cha shari, na kujikinga nayo ni chanzo cha kheri.

Kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama kuchukia wakati yanapofanyika maharamisho yake ni miongoni mwa hasira nzuri.

Kurudia maneno wakati wa haja mpaka ayaelewe msikilizaji na atambue umuhimu wake.

Ubora wa kuomba usia kutoka kwa msomi.

التصنيفات

Tabia njema.