إعدادات العرض
Mche Mwenyezi Mungu popote ulipo, na ovu lifuatishe jema litalifuta, na ishi na watu kwa tabia njema
Mche Mwenyezi Mungu popote ulipo, na ovu lifuatishe jema litalifuta, na ishi na watu kwa tabia njema
Kutoka kwa Abuu Dharri, Jundubi bin Junada, na Abuu Abdulrahman, Muadhi bin Jabali radhi za Allah ziwe juu yao kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Mche Mwenyezi Mungu popote ulipo, na ovu lifuatishe jema litalifuta, na ishi na watu kwa tabia njema"
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහල Македонски नेपाली دری پښتو Shqip ગુજરાતી ភាសាខ្មែរ Українська Čeština Magyar Српски ქართული ਪੰਜਾਬੀالشرح
Ameamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo matatu: La kwanza: Kumuogopa Mwenyezi Mungu na hii inakuwa kwa kutekeleza wajibu, na kuacha maharamisho, katika kila mahali na nyakati na hali, katika siri na wazi, na wakati wa afya na balaa na mengineyo. La pili: Ukiangukia katika ovu, basi fanya baada yake jambo jema kama swala na sadaka na wema na kuunga udugu na toba na mengineyo, kwani hayo hufuta madhambi. La tatu: Ishi na watu kwa tabia njema, kama kutabasamu katika nyuso zao, na upole na ulaini na kutenda wema na kuacha maudhi.فوائد الحديث
Fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake kwa kuwahurumia na kuwasamehe na kuwafutia makosa.
Hadithi imekusanya haki tatu: Haki ya Mwenyezi Mungu ya kuogopwa, na haki ya nafsi kwa kufanya mema baada ya mabaya, na haki ya watu wengine kwa kuishi nao kwa tabia njema.
Himizo la kufanya mema baada ya maovu na kuwa na tabia njema ni miongoni mwa sehemu ya uchamungu, isipokuwa alitaja peke yake kwa sababu ya haja ya kuliweka wazi.
التصنيفات
Tabia njema.