إعدادات العرض
Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu
Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu
Imepokewa Kutoka kwa Shaddad bin Ausi -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mambo mawili niliyahifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu, mtakapoua basi ueni kwa namna iliyokuwa nzuri, na mtakapochinja basi kwa namna iliyokuwa nzuri, na anoe mmoja wenu zana yake ya kuchinjia, na akistareheshe kichinjwa chake".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tagalog ئۇيغۇرچە Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ Русский Deutsch 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip සිංහල دری Svenska አማርኛ Čeština Fulfulde ગુજરાતી Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy Nederlands or Română Kinyarwanda Српски тоҷикӣ ไทย O‘zbek Yorùbá Moore नेपाली Oromoo Wolof Soomaali Български Українська Azərbaycan bm ქართული lnالشرح
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibishia kutenda wema katika kila kitu, na wema: Ni kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu daima, na katika ibada zake, na katika kutenda kheri na kuacha kuwaudhi viumbe, miongoni mwa hayo ni kutenda wema katika kuuwa na kuchinja. Wema katika kuuwa ni wakati wa kisasi: Achague njia nyepesi na rahisi zaidi na ya haraka zaidi kutoa roho kwa mwenye kuuawa. Na wema katika kuchinja ni wakati wa kuchinja: Amuhurumie mnyama kwa kunoa kifaa, na kisinolewe mbele ya mnyama akitazama, na asichinjwe hali yakuwa wanyama wenzake wanatazama.فوائد الحديث
Huruma ya Mwenyezi Mungu na upole wake kwa viumbe.
Wema wa kuuwa na kuchinja uwe kwa namna ya kisheria.
Ukamilifu wa sheria na kushughulikia kwake kila kheri, na miongoni mwake ni kuwahurumia wanyama na upole juu yao.
Katazo la kusulubu (kumtesa) mwanadamu baada ya kumuua.
Uharamu wa kila chenye kumtesa mnyama.