Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze

Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze, na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu jirani yake, na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu mgeni wake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mja mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho ambayo ndani yake kuna marejeo yake na malipo ya matendo yake, basi imani yake inamuhimiza kufanya mambo haya. La kwanza: Kauli njema: Kama tasbihi (kusema: Sub-haanallah) na tahlili (Laa ilaaha illa llaah) na kuamrisha mema, na kukataza mabaya, na kuwasuluhisha watu, ikiwa hatofanya hivyo basi ashikamane na ukimya, na ajizuie na maudhi yake, na ahifadhi ulimi wake. La pili: Kumkirimu jirani: Kwa kumtendea wema na kutomuudhi. La tatu: Kumkirimu mgeni anayekuja kukutembelea: Kwa maneno mazuri na kumlisha chakula na mfano wa hayo.

فوائد الحديث

Imani ya Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho ndio msingi wa kila kheri, na ni msukumo wa kufanya kheri.

Tahadhari dhidi ya maafa ya ulimi.

Dini ya Uislamu ni dini ya ukaribu na ukarimu.

Mambo haya ni katika vipengele vya imani na ni katika adabu njema.

Maneno mengi yanayeweza kumvuta mtu katika machukizo au uharamu, na kusalimika na hilo ni kutozungumza ila katika kheri.

التصنيفات

Tabia njema.