Asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii

Asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii

Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa asiyewahurumia watu naye Mwenyezi Mungu Mtukufu hamhurumii, huruma ya mja kwa viumbe ni katika sababu kubwa za kupata huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

فوائد الحديث

Huruma inahitajika kwa viumbe wote, lakini wametajwa watu kama sehemu ya kuwapa kipaumbele.

Mwenyezi Mungu ndiye Mwingi wa huruma na anawahurumia waja wake wenye huruma, kwani malipo huendana na matendo.

Huruma kwa watu inakusanya kuwafikishia kheri na kuwazuilia shari na kuamiliana nao kwa wema.

التصنيفات

Tabia njema.