Mtu hawi na nguvu kwa kupigana miereka, bali mwenye nguvu ni yule anayeimiliki nafsi yake wakati wa hasira

Mtu hawi na nguvu kwa kupigana miereka, bali mwenye nguvu ni yule anayeimiliki nafsi yake wakati wa hasira

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mtu hawi na nguvu kwa kupigana miereka, bali mwenye nguvu ni yule anayeimiliki nafsi yake wakati wa hasira".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa nguvu halisi si nguvu za mwili,au yule anayemdondosha mwenzake katika wenye nguvu, bali mwenye nguvu na mkali ni yule aliyepambana na nafsi yake na akaitenza nguvu wakati hasira inapokuwa kali; kwa sababu hili linaonyesha uwezo wa nguvu za kuidhibiti nafsi yake na kumshinda kwake Shetani.

فوائد الحديث

Fadhila za upole na kudhibiti nafsi wakati wa hasira, nakuwa hili ni katika matendo mema ambayo uislamu umeyahimiza.

Kupambana na nafsi wakati wa hasira ni zaidi ya kupambana na adui.

Uislamu umebadili mtazamo wa nguvu wa enzi za ujinga kuwa ni tabia njema, hivyo, mtu mwenye nguvu zaidi kuliko wote ni yule mwenye kumiliki uongozi wa nafsi yake.

Kujiweka mbali na hasira; kwani husababisha madhara kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii nzima kwa ujumla.

التصنيفات

Tabia njema.