Muumini si msemaji watu vibaya wala mtoaji wa laana wala muovu wala mwenye kauli chafu

Muumini si msemaji watu vibaya wala mtoaji wa laana wala muovu wala mwenye kauli chafu

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini si msemaji watu vibaya wala mtoaji wa laana wala muovu wala mwenye kauli chafu"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa si katika mambo ya muumini mwenye imani kamili kuwa mtoa aibu za watu katika nasaba zao, wala mwingi wa matusi na laana, wala muovu wa vitendo na kauli ambaye hana haya.

فوائد الحديث

Kukanushwa imani katika dalili za kisheria hakuwi isipokuwa kwa kutenda kitendo cha haram au kuacha wajibu.

Himizo la kuhifadhi viungo na kuvilinda na mabaya, hasa hasa ulimi.

Amesema As-Sanadi: Na katika tamko la kusisitiza katika kauli yake (Mwingi kutukana, na mwingi wa kutoa laana) Ni dalili kuwa kutoa matusi na laana mara chache si vibaya kwa mtu atakayestahiki hilo, na wala haidhuru mtu kusifika kwa sifa za waumini.

التصنيفات

Tabia njema., Adabu ya mazungumzo na kunyamaza.