Fanyeni mambo kuwa mepesi na wala msiyafanye kuwa magumu, na wapeni watu bishara njema na wala msiwakimbize

Fanyeni mambo kuwa mepesi na wala msiyafanye kuwa magumu, na wapeni watu bishara njema na wala msiwakimbize

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fanyeni mambo kuwa mepesi na wala msiyafanye kuwa magumu, na wapeni watu bishara njema na wala msiwakimbize".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwafanyia wepesi watu na kutowafanyia ugumu katika mambo yote ya Dunia na Akhera, na hili liwe katika mipaka aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu na sheria. Na anahimiza kuwapa bishara kwa kheri, na kutowakimbiza.

فوائد الحديث

Wajibu wa muumini ni kuwavutia watu kwa Mwenyezi Mungu na kuwahamasisha katika kheri.

Ni wajibu kwa mwenye kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu atazame kwa hekima namna sahihi ya kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu.

Kutoa habari njema huleta furaha na watu kuelekea na kutulizana kwa mlinganiaji na yale anayowafundisha watu.

Kuwatia ugumu watu husababisha kuwachukiza watu na kuwakimbiza, na kuyatia shaka maneno ya mfikishaji.

Upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake nakuwa Yeye ameridhia kwao dini ya upole na sheria nyepesi.

Wepesi ulioamrishwa ni ule uliokuja katika sheria.

التصنيفات

Tabia njema.