Kwa hakika nimetumwa ili kutimiliza tabia njema

Kwa hakika nimetumwa ili kutimiliza tabia njema

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kwa hakika nimetumwa ili kutimiliza tabia njema"

[Ni nzuri]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba, hakika Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alimtuma yeye ili akamilishe mambo bora na tabia zilizo njema; kiasi kwamba alitumwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili atimize yale waliyokuwa nayo Mitume, na alikuja kukamilisha tabia njema za waarabu, kwani walikuwa wakipenda kutenda kheri na wakichukia shari, walikuwa ni watu wenye utu na ukarimu na utukufu; akatumwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili kukamilishe mapungufu yaliyoko katika tabia zao, kama kujifaharisha kwao kwa nasaba, na kujikweza na kumdharau fakiri na nyinginezo.

فوائد الحديث

Himizo la kuwa na tabia njema, na katazo la kinyume chake.

Kumebainishwa umuhimu wa tabia njema katika sheria ya Uislamu na kwamba ni katika vipaumbele vyake.

Watu wa zama za ujinga walikuwa na mabaki ya tabia njema, ikiwemo ukarimu na ushujaa na mengineyo, Uislamu ukaja kuyakamilisha.

التصنيفات

Tabia njema.