إعدادات العرض
Kamwe!, Usidharau chochote katika wema, hata kama ni kukutana na ndugu ukiwa na uso mkunjufu
Kamwe!, Usidharau chochote katika wema, hata kama ni kukutana na ndugu ukiwa na uso mkunjufu
Kutoka kwa Abuu Dhari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kamwe!, Usidharau chochote katika wema, hata kama ni kukutana na ndugu ukiwa na uso mkunjufu".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ Deutsch 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە සිංහල ไทย دری Fulfulde Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių or Română Kinyarwanda Српски O‘zbek Moore नेपाली Oromoo Wolof Soomaali Malagasy Български Українська Azərbaycan ქართული Lingala bm тоҷикӣ Македонскиالشرح
Amehimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kutenda wema, na mtu asiudharau hata kama utakuwa kidogo, na miongoni mwake ni ukunjufu wa uso kwa kutabasamu wakati wa kukutana, ni lazima kwa muislamu alipupie hilo; kwa sababu hujenga kuwa na ukaribu na ndugu yako muislamu na huingiza furaha kwake.فوائد الحديث
Fadhila za kupendana kati ya waumini, na kutabasamu na bashasha wakati wa kukutana.
Ukamilifu wa sheria hii na kugusa kwake kila sekta, nakuwa imekuja na mambo yote ambayo yana masilahi kwa waislamu na kuunganisha umoja wao.
Himizo la kutenda wema hata kama ni kidogo.
Inapendeza kuingiza furaha kwa waislamu; kwani ndani yake kuna kuleta ukaribu baina yao.
التصنيفات
Tabia njema.