إعدادات العرض
Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote halitomdhuru dhambi lolote kwa hilo, na atakayekufa na hali yakuwa anamshirikisha, basi hakuna jema litakalomnufaisha
Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote halitomdhuru dhambi lolote kwa hilo, na atakayekufa na hali yakuwa anamshirikisha, basi hakuna jema litakalomnufaisha
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- anasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote halitomdhuru dhambi lolote kwa hilo, na atakayekufa na hali yakuwa anamshirikisha, basi hakuna jema litakalomnufaisha".
[Sahihi] [Imepokelewa na Ahmad]
الترجمة
العربية Português دری Македонски Magyar Tiếng Việt ქართული Kurdî বাংলা ไทย অসমীয়া Nederlands ਪੰਜਾਬੀ Bahasa Indonesiaالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekufa na akakutana na Mwenyezi Mungu akiwa na tauhidi hamshirikishi na chochote basi huyo ni katika watu wa Peponi, hata kama akiadhibiwa kwa dhambi motoni, na atakayekufa huku akimshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote hakuna jema lolote litakalomnufaisha; na Pepo kwake ni haramu.فوائد الحديث
Tahadhari dhidi ya ushirikina, na kwamba hilo ni katika madhambi na makosa makubwa, na kwamba Mwenyezi Mungu haisamehe.
Fadhila ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na kwamba hilo linawajibisha kuingia Peponi; hata ikiwa baada ya kuadhibiwa.
Umuhimu wa kudumu katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu mpaka kufa, na kutofanya kinyume chake ambacho ni ushirikina.
