Tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ananong'ona na Mola wake, msiudhiane baadhi yenu kwa baadhi

Tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ananong'ona na Mola wake, msiudhiane baadhi yenu kwa baadhi

Kutoka kwa Abuu Saidi -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikaa itikafu Mtume rehema na amani ziwe juu yake msikitini, akawasikia wakidhihirisha kisomo, akafunua pazia, akasema: "Tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ananong'ona na Mola wake, msiudhiane baadhi yenu kwa baadhi, na wasinyanyue sauti baadhi yenu kwa wenzao katika kisomo", au alisema: "Katika swala".

[Sahihi] [Imepokelewa na Abuu Daud]

الشرح

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekaa itikafu katika kuba (hema) ndani ya msikiti wake kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, akasikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake wakidhihirisha kisomo chao cha Qur'ani kwa sauti kubwa inayowaudhi baadhi yao. Akafunua pazia la hema, na akamlaumu aliyefanya hivyo na hakupendezwa, na akasema: Nyinyi wote mnazungumza na Mola wenu kwa kusoma kwenu Qur'ani, basi mmoja wenu asimuudhi mwenzake kwa sauti yake katika kusoma kwake, au ndani ya swala yake.

فوائد الحديث

Katazo la kunyanyua sauti kwa kusoma Qur'ani, ikiwa inamuudhi mtu.

Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwafundisha Maswahaba zake adabu za kusoma Qur'ani.

التصنيفات

Adabu za usomaji wa Qur'an.