Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba

Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba.

[Ni nzuri] [رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد]

الشرح

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwafundisha Maswahaba zake Qur'ani na akiwasomesha yeye mwenyewe katika hali zote madam hajawa katika hali ya janaba litokanalo na tendo la ndoa kwa wakeze.

فوائد الحديث

Kutofaa kusoma Qur'ani kwa mwenye janaba mpaka aoge.

Kufundisha kwa vitendo.

التصنيفات

Hukumu za Qur'an na Misahafu., Adabu za Usomaji Qur;an na Ubebaji wa Qur'an., Kuoga.