إعدادات العرض
1- Kiliwekwa kwaajili ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chombo cha kuogea janaba, akamimina kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto mara mbili -au tatu- kisha akaosha tupu yake, kisha akapiga ardhi kwa mkono wake
2- Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapooga janaba, anaosha mikono yake kisha anatawadha udhu wake wa swala kisha anaoga
3- Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake
4- Nilimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kuwa muislamu, akaniamrisha nioge kwa maji na mkunazi