Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge

Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge

kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anasisitiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa atakayetaka kuja kwa ajili ya swala ya Ijumaa basi inapendeza kwake kuoga, mfano wa kuoga kwake josho la janaba.

فوائد الحديث

Mkazo wa kuoga kwa ajili ya Ijumaa, nakuwa hilo ni sunna kwa muumini siku ya Ijumaa na ikiwa wakati anataka kwenda kuswali ndio bora zaidi.

Kutilia manani swala la usafi na harufu nzuri ni katika tabia njema za muislamu na adabu zake, na amri inakuwa na mkazo zaidi wakati wa kukutana na watu na kukaa nao, hasa hasa katika mikusanyiko na swala za jamaa.

Tamko katika hadithi linamuhusu mwenye uwajibu wa kuswali Ijumaa; kwa sababu yeye ndiye anayekwenda kuswali.

Ni lazima kwa mwenye kwenda katika swala ya Ijumaa awe msafi, aoge ili harufu iondoke katika mwili wake na ajitie manukato, na ikiwa atatawadha pekee pia itatosha.

التصنيفات

Kuoga., Swala ya Ijumaa