Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake

Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake

Na imepokelewa katika sahihi Bukhari kutoka kwa Abuu Huraira Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni haki iliyotiwa mkazo kwa kila muislamu aliyebalehe mwenye akili timamu aoge katika kila siku saba za wiki siku moja, aoshe katika siku hiyo kichwa chake na mwili wake, kwa kutafuta twahara na usafi, na siku bora katika siku hizi ni siku ya Ijumaa, kama inavyojulikana kutoka katika baadhi ya riwaya, na kuoga siku ya Ijumaa kabla ya swala ni sunna iliyotiwa mkazo, hata kama atakuwa alioga siku ya Alhamisi kwa mfano, na kinachoiondoa katika uwajibu ni kauli ya Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake-: "Watu walikuwa wakifanya kazi na shughuli mbali mbali za kimaisha, na walikuwa wanapokwenda katika Ijumaa wanakwenda katika muonekano wao huo huo: Wakaambiwa: Basi mngeoga (Ingekuwa kheri)", kaipokea Bukhari, na katika riwaya yake nyingine: "Wakiwa na harufu" Yaani: Harufu ya jasho na mfano wake, lakini pamoja na hivyo wakaambiwa (Lau mgeoga ingekuwa bora), hivyo kwa wasiokuwa Masahaba wanahaja kubwa ya kulitekeleza hili.

فوائد الحديث

Kutilia umuhimu na kujali kwa Uislamu swala la usafi na twahara.

Kuoga siku ya Ijumaa kumependekezwa sana tena kwa mkazo kwa ajili ya swala.

Kimetajwa kichwa, pamoja nakuwa kutajwa mwili kungetosha kukusanya na kichwa; Lakini ni kwa ajili ya kukitilia maanani.

Ni wajibu kuoga kwa kila aliyepatwa na harufu mbaya, inayo waudhi watu.

Siku muhimu zaidi kwa ajili ya kuoga ni siku ya Ijumaa; kwa sababu ya fadhila zake.

التصنيفات

Kuoga.