إعدادات العرض
Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapooga kwa ajili ya janaba, anaosha mikono yake, na anatawadha udhu wake ule wa swala, kisha anaoga
Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapooga kwa ajili ya janaba, anaosha mikono yake, na anatawadha udhu wake ule wa swala, kisha anaoga
Imepokewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapooga kwa ajili ya janaba, anaosha mikono yake, na anatawadha udhu wake ule wa swala, kisha anaoga, kisha anaachanisha nywele zake kwa mkono wake, mpaka pale anapohisi kuwa ngozi yake yote imeenea maji, anajimwagia maji kwa michoto mitatu, kisha anaosha mwili wake wote uliobakia, na Aisha akasema: Nilikuwa nikioga mimi na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja, tukichota sote katika chombo hicho.
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी Português Kurdî සිංහල Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ئۇيغۇرچە Tiếng Việt Hausa ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or नेपाली Malagasy Kinyarwanda తెలుగు Lietuvių Oromoo Română മലയാളം Nederlands Soomaali Српски Українська Deutsch ಕನ್ನಡ Wolof Moore Shqip ქართული Azərbaycan Magyar বাংলাالشرح
Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuoga janaba anaanza kwa kuosha mikono yake, kisha anatawadha kama anavyotawadha udhu wa swala, kisha anajimwagia maji katika mwili wake kisha anaachanisha nywele za kichwa chake kwa mikono yake, mpaka anapohisi kuwa maji yamefika katika maoteo ya nywele zake, na yameloanisha ngozi, anajimwagia maji kichwani mara tatu kisha anaosha mwili mzima. Na akasema Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikioga mimi pamoja na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutoka katika chombo kimoja, tukichota sote.فوائد الحديث
Josho lina aina mbili: Linalotosheleza na lilokuwa kamili, ama josho linalotosheleza ni mtu kunuia twahara, kisha akaeneza maji katika mwili wake ikiwa ni pamoja na kupandisha maji puani na kusukutua, na ama josho lilokuwa kuwa kamili ataoga kama alivyo oga Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithi hii.
Neno Janaba hutumika kwa kila aliyetoa manii, au kafanya tendo la ndoa hata kama hajamtoka.
Inaruhusiwa mwanandoa kutazama uchi wa mwenzake, na kuoga pamoja katika chombo kimoja.
التصنيفات
Kuoga.